- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NAMBA YA JELA YA SUGU YAMCHANGANYA SPIKA NDUGAI
Dar es salaam: Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugui amekosa uvumilivu juu ya muonekano wa mavazi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kuwa na Lebo yenye muonekano wa namba zinazofanana kwenye kila suti anayovaa mbunge huyo, Ndipo spika akahoji kwa kutaka kufahamu kwa nini pamoja na kuvaa suti nzuri lakini bado zinaonekana na namba ambazo hazieleweki eleweki.
Spika Ndugai ameyaongea hayo Leo June 5, 2018 wakati Mbunge huyo akichangia mchango wake katika bajeti ya wizara ya fedha na mipango kwa mwaka wa fedha 2018/2019. "Kabla sijakuongezea dakika moja waheshimiwa wengi wameniandikia kwamba umevaa suti nzuri sana lakini umeweka lebo za ajabu hiyo 219 ni kitu gani? alihoji Spika Ndugai
Sugu akamjibu spika "Hii ni namba yangu ya mfungwa jela, ambayo nitaendelea kuvaa kadiri ambavyo nitajisikia. Kuhusu Suti Mh. Spika wewe unanijua ni kawaida yangu kupiga suti kali".
Aidha Mh Spika ameahidi kulifanyia kazi swala la Mbunge huyo kufuatilia zaidi kwenye kanuni zake kama inaruhusiwa kuvaa namba za magereza ndani ya jengo la Bunge.
Sugu amekuwa akionekana akivaa nguo zenye namba 219 mbele ambapo huwa akifafanua kwamba ilikuwa namba yake siku alipoingia magereza ya Ruanda baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi 5 kwa kosa la kutoa lugha chafu dhidi ya Rais Magufuli