- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NDITIYE ANUSURIKA KUFA
Singida: Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amepata ajari ya gari leo katika eneo la Iguguno mkoani Singida wakati akielekea Dodoma.
Kwamujibu wa MCL linasema limezungumza na kiongozi huyo ambaye amesema katika ajali hiyo hakuna mtu aliyepata madhara baada ya gari hiyo kupinduka zaidi ya mara nne.
“Kwenye gari tulikuwa watu saba na mtoto mmoja, nashukuru Mungu hakuna madhara ya mtu kuumia wote tupo salama licha ya kuwa gari lilibinuka zaidi ya mara nne,” alisema Nditiye kwa njia ya simu.
Aidha, picha ya video inayosambaa katika mitandao ya kijamii inaonyesha gari hilo ambalo lilikuwa linapeperusha bendera ya taifa likiwa pembezoni mwa barabara limeharibika vibaya bila kuwa na tairi moja la mbele upande wa kulia.