- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NS UTALII, JAPHET HASUNGA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA TFS KANDA YA KUSINI
MTWARA: Watumishi wa Wakala wa Huduma Tanzania (TFS)wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na sheria za utumishi wa Umma ili kuleta ufanisiwakati wanapotekeleza majukumu yao ya uhifadhi.
Rai hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati alipowatembelea watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS)kanda ya Kusini kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi yasiku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii
Amewataka kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu na yeyote atakayetuhumiwa kupokea rushwa hata kama hajapokea rushwa hiyo kutoka wafugaji kwa makubaliano ya kuingiza mifugo hifadhini kwa makubaliano ya malipo atashughulikiwa ipasavyo.
Aliongeza kuwa endapo watumishi hao wataweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo hakuna kiongozi yeyote watakayesumbuana nao
‘’Tunataka mfanye kazi zenu za uhifadhikwa weledi wa hali ya juu na mkifanya vizuri basi nakuwa nimefanya mimi na mkifanya vibaya mnakuwa mnaniangusha mimi hivyo sitokubali’’ alisisitiza Naibu Waziri Hasunga.
Aidha, Amewata wafanye kazi kwa kushirikiana na jamii kwa vile hakuna shughuli yeyote itakayofanikiwa endapo wananchi wataachwa nyuma.
‘’Tunataka jamii ione faida ya moja kwa moja kwa kupata elimu kuhusu uhifadhi pamoja na kushirikishwa kwenye masuala yote ya misitu ili waweze kutoa ushirikiano wakati ukataji miti unapofanyika popote pale’’
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo amewataka watumishi hao kuchukua likizo kila mwaka na kuitumia likizo hiyo kwenda sehemu mpya kutalii na kupumzisha akili na kujifunza vitu vipya baadala ya kila likizo kwenda kijiji walikozaliwa kama ilivyozoeleka kwa watumishi wengi.
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu, Kanda ya Kusini,Ebramtino Mgiye alimweleza Naibu Waziri huyo kuwalicha ya kuwa nachangamoto ya uhaba wa vitendea kazi lakini kila mtumishi kwa nafasi yake amekuwa akitimiza wajibu wake.