- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NAIBU WAZIRI SHONZA AIPA TBC SIKU 10 KUFUNGA MITAMBO LONGIDO
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amelipa siku 10 Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Kanda ya Kaskazini kukamilisha mara moja ujenzi wa kituo cha kurusha matangazo kinachojenga Makao Makuu ya Wilaya ya Longido.
Mheshimiwa Shonza ametoa agizo hilo leo Wilayani Longido alipotembelea kituo cha kurusha matangazo ya TBC kinachojengwa Wilayani hapo kwa lengo la kutatua kero ya kukosekana kwa usikivu wa matangazo ya TBC ambapo wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakisikiliza radio za nchi jirani na hiyo imewafanya kukosa taarifa zenye ukweli na uhakika za ndani ya nchi.
“Chumba hichi cha kuhifadhi busta na mitambo mingine ni kidogo sana na ujenzi wake siyo wa kuchukua muda mrefu hakikisheni mpaka Januari 10,muwe mmekamilisha ujenzi wa Kituo hichi wananchi wa Longido wanakiu kubwa ya kutaka kusikia matangazo kutoka chombo hichi cha serikali chenye habari za ukweli na uhakika na hii ni haki yao,”alisema Mhe.Shonza.
Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo aliwasisitiza viongozi hao wa TBC kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho cha kurushia matangazo kinajengwa kwa kutumia vifaa imara kwani serikali ilitenga bajeti yenye fedha za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha usikivu unaboreshwa katika maeneo ya mipakani na malengo ya serikali ni kabla ya mwa 2020 kero hii ya usikivu iwe imekwisha.
Kwa Upande wa Katibu Tawala Wilaya ya Longido Bw.Toba Nguvila asisitiza kuwa ukosekanaji wa usikivu wa Matangazo ya TBC Wilayani hapo umekuwa ni changamoto kubwa kwa utoaji na upokeaji wa taarifa muhimu kuhusu shughuli za kiserikali kwani wakazi wa eneo hilo wanashindwa kupata taarifa hizo kwa wakati ukizingatia jamii ya wakazi hao ni wafugaji na huishi kwa kuhama hama.
“Tungependa matangazo ya TBC yaanze kusikika hapa Longido haraka kwani yapo mambo mengi yanayohitajika kutolea elimu kwa wakazi wa eneo hili kupitia vipindi vya redio ,kwani TBC ni chombo kinacho rusha habari zenye ukweli na uhakika hivyo tungependa wananchi wa hapa nao waweze kusikia matangazo yenu, ”alisema Bw.Nguvila.
Pamoja na hayo nae Meneja wa TBC Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso alieleza kuwa ameyapokea maelekezo hayo na atahakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya muda na vifaa vyake kuwa veye ubora.
Hata hivyo meneja huyo aliwahakikishia viongozi hao mara baada ya kukamilika ufungwaji wa mitambo hiyo usikivu wa matangazo katika eneo hilo utakuwa uko imara.