Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:38 pm

NEWS: NAIBU WAZIRI MANYANYA TEKLONOJIA ITACHANGIA KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA.

ILI kufikia uchumi wa kati na wa Viwanda teklonojia imetajwa kuwa ni njia mojawapo ambayo itaisaidia jamii kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda Mhe. Injinia Stella Manyanya wakati akifungua rasmi mkutano kwa njia ya Mtandao yaani (Video Conference) wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Mamlaka za mikoa na Halmashsauri za Wilaya kuhusu masuala ya sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na taasisi zake uliofanyika leo mjini Dodoma.

Manyanya amesema teklonojia itasaidia katika kurahisisha mawasilano ambapo mtu hutumia muda mchache katika kutekeleza majukumu yake yanayohusuka katika mtandao mtandao.


Mbali na hayo Mhe. Naibu Waziri amewashukuru Makatibu Tawala wa Mikoa, Wasaidizi wao na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya pamoja na wataalamu na maafisa mbalimbali kwa kuitikia wito wa kuungana pamoja ili kubuni njia rahisi na nyepesi ya kufikisha taarifa kwa haraka katika jamii.

Wizara ilianza na taasisi yake ya BRELA ambayo ilielezea majukujumu yake na huduma mbalimbali wanazotoa kwa umma na kutoa fursa ya wadau kutoka mikoa yote iliyoshiriki ikiwemo Mbeya, Songwe, Kilimanjaro, Ruvuma, Kigoma, Lindi, Singida, Pwani na Dodoma walipata fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa papo kwa papo.