- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NAIBU WAZIRI AITAKA JAMII KUWASAIDIA WALEMAVU.
DOM: Jamii imetakiwa kuwa na utayari wa kujitolea bila kuchoka kwa watu wenye mahitaji maalum hususani walemavu ili kuwapa fursa ya ushiriki katika ustawi wa Taifa.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe Anthony Mavunde wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Chuo Kikuu Cha Dodoma Mkoani hapa.
Aidha Mavunde amesema ,jamii imekuwa ikijisahau kutoa huduma kwa watu wenye uhitaji jambo linalopaswa kupingwa na kuanza kuwajibika kwa hali na Mali ili kufanikisha mahitaji yao ikiwemo elimu.
Akiendelea kufafanua amesema ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kutetea matatizo ya wanyonge na kuyaishi ,sharti jamii ishirikiane bega kwa bega bila kutizama itikadi za dini na siasa na kutatua changamoto za watu wasiojiweza.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mavunde amekabidhi kiti cha magurudumu mawili kilichotolewa na hospitali ya benjamini Mkapa kwa mtoto Cristopher Elias mwenye umri wa miaka kumi akitokea kijiji cha Mtitaa wilayani Bahi Mkoa hapa ambaye amekamatwa miguu yote miwili kufuatia maradhi ya miguu yaliyokuwa yakikamkabili.
ββ "Mimi kama binadamu lakini pia waziri ninayehudumu ofisi ya waziri mkuu natamani kuona mtoto huyu anafikia malengo yake kielimu hivyo nimeagiza madaktari kuchukua vipimo kwa ajili ya kumtengenezea miguu ya bandia, nina imani kwa kiasi fulani atafarijika japo ni vigumu kuhimili vishindo hivi lakini pia nitamfanya kuwa sehemu ya familia yangu ," amesema Mavunde .
Awali akizungumza Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa DkAlphonce Chandika amesema uongozi wa hospitali hiyo uliafikiana na kuona umuhimu wa kumpa faraja mtoto huyo katika kipindi hiki kigumu kwake.
Hata hivyo DkChandika amesema,walifikia maamuzi ya pamoja kumpatia mtoto huyo kiti cha kutembelea (wheel chair)kwa kuwa wanatambua kuwa ni jukumu la kila mwanajamii kubeba mizigo ya watu wengine
"Kila mwanajamii akishiriki kujitoa kwa uaminifu kuwasaidia wasiojiweza ,itasaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea mabadiliko kiuchumi kwani hakutakuwa na nguvu ya utegemezi katika taifa letu," amesema Dk huyo.
Hospitali ya Benjamini Mkapa inaendela na hatua ya pili ya upandikizaji figo ambapo hatua ya kwanza ilifanyika mwezi marchi 22 mwaka huu na kufanikiwa na hadi leo ikitarajiwa kufanya oparesheni nyingine mbili na kuwa na jumla ya operesheni nne tangu hospitali hiyo ianze kutoa huduma hiyo