- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : NABIL SADEK ATOA AMRI YA KUKAMATWA 29 KWA KUIFANYIA UJAJUSI UTURUKI
Mwendesha mashtaka mkuu wa Misri ametoa amri wa kutiwa mbaroni watu 29 na kushikiliwa kwa muda wa siku 15 za uchunguzi kwa madai ya kuifanyia ujasusi Uturuki na kujiunga na kundi moja la kigaidi.
Mwendesha mashtaka nchini misri Nabil Sadek
Taarifa ya ofisi ya mwendesha mashtaka huyo mkuu wa Misri imesema kuwa, watu hao 29 pamoja na wengine ambao hawajapatikana wanakabiliwa na tuhuma za kuifanyia ujasusi Uturuki na kuwa wanachama wa kundi moja la kigaidi.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwapa raia wa Misri huduma za simu za kimataifa ambazo zilikuwa zimetegeshewa vifaa vya kufanya ujasusi dhidi ya Misri kwa maslahi ya Uturuki
Maandamano ya kupinga serikali nchini misri
Watu hao wanadaiwa kuwa, walikuwa wakisikiliza kwa siri mazungumzo ya simu ya raia hao wa Misri ili kupata maoni yao na kupeleka taarifa hizo kwa mashirika ya kijasusi ya Uturuki.
Taarifa ya ofisi hiyo imedai kuwa watuhumiwa hao walifanya kazi zao kwa makubaliano na majasusi wa Uturuki na wanachama wa kundi la kimataifa la Ikhwanul Muslimin ili kulisaidia kundi hilo kutwaa madaraka nchini Misri.
Watuhumiwa hao wanakabiliwa pia na tuhuma za kutakatisha fedha, kufanya biashara ya fedha kinyume cha sheria na kushirikiana na vyombo vya habari vya nje kueneza habari za uongo dhidi ya serikali ya Misri.
Uhusiano wa Misri na Uturuki uliharibika tangu baada ya jeshi la Misri kumpindua Rais Muhammad Morsi mwaka 2013. Uturuki ililaani vikali jambo hilo na kusema hayo yalikuwa ni mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais aliyechaguliwa kwa kura za wananchi.