- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWILI WA SISTER ALIYEJIUA KWA KUJITUPA GHOROFANI KUZIKWA
Mwanza: Mwili wa mtawa Suzan Bathlomeo (48) aliyefariki juzi kwa kujirusha kutoka ghorofani katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza ulisafirishwa jana kwenda Bukoba, Kagera kwa ajili ya maziko
Kwamujibu wa ofisa uhusiano wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Lucy Mogela alisema misa hiyo ilifanyika katika Kanisa Katoliki Bugando kabla ya kuanza safari. Kuhusu taratibu za mazishi na taarifa nyingine muhimu, Lucy alisema zitatolewa na msemaji wa shirika la watawa la Mtakatifu Theresia lililopo mjini Bukoba.
Hata hivyo, kamanda wa polisi mkoani hapa, Jonathan Shanna alisema juzi kuwa uchunguzi umebaini ofisi aliyokuwa akifanyia kazi mtawa huyo kuna tuhuma za upotevu wa zaidi ya Sh300 milioni zilizosababisha watumishi wenzake wanane kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi na baadhi kufukuzwa.