- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWENYEKITI WA UVCCM AGONGA MWAMBA MAHAKAMANI.
DODOMA: Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dodoma imetupilia mbali ombi la dhamana ya aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Sadifa Khamis (35) .
Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Emmanuel Fovo ametupilia mbali ombi hilo jana lililoombwa kwa upande wa utetezi nakusema kuwa uchunguzi bado unaendelea.
Amesema kuwa kutokana na uchunguzi unaoendelea kufanywa na TAKUKURU mshitakiwa ataendelea kukaa rumande mpaka desemba 19 mwaka huu ambapo kesi hiyo itasikilizwa tena na kutolewa maamuzi.
Akisoma mashtaka yanayomkabili mwenyekiti huyo kupitia jarida kesi namba 232 wakili wa serikali Biswalo Biswalo akishirikiana na wakili Stanley Luoga alisema kuwa mshitakiwa anakabiliwa na makosa mawili ya rushwa.
Amesema kosa la kwanza ni mtuhumiwa akiwa katika eneo analoishi la kata ya mnadani mjini hapa alitoa rushwa ya Vinywaji kwa Kadogo Shabani,Abdalah Hamimu,Octavian Andrea,Didas Zimbihile,Yasinta Nyamwiza,na John Lufunga.
Wengine ni Mtwawafu Kantangayo,Haleluya Ivody,Deocres Kagunila,Emmanuel Shitobelo,Happiness Rynyogote,Adole Andrew,Adinan Musheruzi,Editha Domisian na Hashim Abdallah ili waweze kumchagua Rashid Mohamed Rashid ambaye alikuwa anagombea umakamu mwenyekiti UVCCM taifa.
Akisoma Shitaka la pili wakili huyo amesema mshitakiwa Sadifa Khamis akiwa katika eneo analoishi la kata ya mnadani alitoa rushwa ya hela ya usafiri kwa watu kutoka Dodoma kwenda Kagera.
Watu hao waliopewa rushwa ni Kadago Shabani,Abdallah Hamimu,Octavian Andrew,Didas Zimbihile,Yasinta Nyamwiza,John lufunga,Mtwawafu Katangayo,Haleluya Ivody,Deocres Kagunila,Emmanuel Shitobelo.
Wengine ni Happines Rynyogote,Adolf Andrew,Adnani Musheruzi, Editha Domisian na Hashim Abdallah wote hawa iliwaweze kumchagua Rashid Mohamed Rashidi aliyekuwa akigombea makamu mwenyekiti taifa UVCCM.
Bisolwa amesema kupitia kifungu cha 15( 1) (b) na (2)cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 anaiomkba mahakama tukufu iendelee kumshikilia mtuhumiwa kwani ataingilia uchaguzi na kuingilia upelelezi unao endelea.
“Mpaka muda huu uchaguzi bado unaendelea kwani niwasiku mbili tarehe 10 na 11 hivyo na mshitakiwa bado hajakabidhi kijiti kwa mteuliwa mpya hivyo basi naiomba mahakama yako iendelee kumshikilia”alisema Bisolwa.
Naye wakili wa kujitegemea wa upande wa mshitakiwa Godfrey Wasonga amesema kuwa mteja wake ni mmbunge na yupo makini katika utendaji wake wa kazi hivyo basi hakuna sababu zilizo na mashiko za kuendelea kumuweka rumande.
Amesema wanapinga maombi ya wakili wa serikali yakutopewa dhamana kwa mteja wake nakusema kuwa dhamana ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
“Kifungu cha 15 (1)(b) na (2)hakizuwii kwa namna yoyote kutokupewa dhamana kwa mteja wangu”amesema Wasonga.
Hata hivyo kwa upande wa mshtakiwa Sadifa Khamis ambaye ameifikishwa mahakamani hapo na gari aina ya Ford T994 BEM alipoulizwa na mahakama kuhusu makosa yanayomkabili alikataa nakusema hajafanya makosa hayo.