- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWENYEKITI WA UCHAGUZI AKANUSHA WAKALA WA CHADEMA KUZUIWA KUINGIA VITUO VYA KURA
Dar es Salaam: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage amekanusha vikali madai yanayotolewa na vyama vya upinzani kwamba mawakala wao wamezuiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura kwenye uchaguzi wa ubunge jimbo la Ukonga na Monduli.
Jaji Kaijage ameyasema hayo leo Jumapili Septemba 16, 2018 alipotembelea kituo cha kupigia kura kilichopo Shule ya Msingi Juhudi katika jimbo la Ukonga, kukiri kuwa idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni ndogo.
Wakati Jaji Kaijage akieleza hayo, mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Monduli, Yonas Laizer amesema mawakala wa chama hicho wamezuiwa kuingia vituoni.
Katika ufafanuzi wake Jaji Kaijage amesema katika majimbo yote ya Monduli na Ukonga uchaguzi ulianza kwa wakati na unaendelea vizuri.
Amesema katika jimbo la Monduli lenye vituo 256 ni mawakala wanne tu ndio walizuiliwa kuingia vituoni, ni kwa sababu za msingi.
"Hao mawakala wanne walizuiliwa kwa kuwa hawakutambuliwa na msimamizi, hawakuapishwa walikwenda kwa niaba ya wengine," amesema.
“Hizi habari zinazosambazwa kuwa mawakala wote Monduli wamezuiwa si kweli watu wasisambaze taarifa ambazo hawana uhakika nazo. Kwenye jimbo la Ukonga lenye vituo vya kupigia kura 673 uchaguzi unaendelea vizuri.”
Amesisitiza, “naona kila kitu kinakwenda sawa hakuna wakala aliyezuiliwa na kama hajafika ni kwa utashi wak