Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:26 am

NEWS: MWENYEKITI WA CCM ABURUZWA MAHAKAMANI KWA KUGHUSHI CHETI

Dar es salaam: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri anayejulika zaidi kama Nora Mzeru amefikishwa mahakamani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, akikabiliwa na mashitaka ya kughushi cheti cha ndoa.

Related image

Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ester Kyara alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule kuwa Mzeru katika siku isiyojulikana jijini Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078 kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na marehemu Silvanus Mzeru Februari 4, 1995 katika Kanisa Katoliki Mburahati, wakati akijua si kweli.

Image result for Nora Mzeru

lakini kwa upande wa Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo baada ya kusomewa mashtaka na Upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo ya jinai namba 601 ya mwaka huu, unaendelea na kwamba hawana pingamizi la dhamana kwa mshitakiwa. Hakimu Haule alimtaka mshitakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, ambao watasaini bondi ya Sh milioni mbili. Mshitakiwa huyo alitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa. Hakimu Haule ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21,mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa.