- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANAMKE ALIYEJIOA MWENYEWE ATAFUTA MSAADA WA ADA WA MASOMO
Mwanamke mmoja ambaye amejichukulia umaarufu Duniani baada ya Kujioa mwenyewe mwezi Agosti mwaka huu Lulu Jemimah, 32, anatafuta msaada wa Dolla $ 10, 194 ili aweze kulipia Ada katika chuo maarufu Duniani cha Oxford, kilichopo nchini Uingereza, Kumalizia mwaka wa pili wa masomo yake ya Uzamili.
Alojioa mwezi Agosti jijini Kampala Uganda ili kuweza kuonesha Jamii kuwa mwanamke anaweza kuishi bila msaada wa mwanae.
Anasema haikuwa dhamira yake kuomba msaada lakini hofu ya kufutwa chuo kutokana na kukosa fedha imemlazimu afanye hivyo.
"Nimepata bahati ya kuwa katika chuo bora chenye wanafunzi makini na walimu wenye weledi mkubwa...Nimefikia hapa kutokana na msaada wa marafiki na watu nisiowafahamu. Kwa mara nyingine tena naomba msaada wenu.
"Nikiwa na miaka 16 baba yangu aliandika hotuba yake kwa ajili ya kuisoma siku ya harusi yangu. Kila nilipokuwa nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa mama yangu alikuwa akiniombea, na kwa miaka ya karibuni maombi yake yalikuwa pamoja na kupata mume bora, ambaye atanifaa," amesema Bi Jemimah.
Kutokana na hali hiyo, Jemimah anasema aliamua kuchukua uamuzi wa kuwatuliza; "Nilipotimiza miaka 32 nikaamua kujioa. Naamini mimi nitajitunza na kujipa amani."
Harusi yake ilimgharimu kiasi cha dola 2 tu ambazo ni gharama yake ya usafiri. Aliazimisha gauni la harusi kwa rafiki, vito kutoka kwa dada yake na keki ya harusi iliokwa na kaka yake.
Waalikwa walitakiwa kujinunulia chakula na vinywaji kwa pesa zao wenyewe.