- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANAMKE AHUKUMIWA MIAKA 12 JELA KWA KUMUUZA MWANAE WA KIUME
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Berrin T. mwenye umri wa miaka 48 mkazi wa nchini Ujerumani amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa kumuuza mwanawe wa kiume mwenye miaka 9 kwa wabakaji kupitia mtandao wa intaneti katika moja ya matukio ya kikatili kabisa kuwahi kushuhudiwa hivi karibuni nchini ujerumani.
Siku ya jana Jumanne (7 Agosti 2018), mahakama ya Freiburg, kusini magharibi mwa Ujerumani, ilimtia hatiani mwanamke huyo aliyetambulishwa kwa jina la Berrin T. mwenye umri wa miaka 48 na mpenziwe wa kiume Christian L. mwenye umri wa miaka 39 kwa makosa yapatayo 60, yakiwemo ya kumlazimisha mvulana huyo kuingia kwenye ukahaba, kumtisha kwa maneno na kumtesa, ubakaji na ukatili uliopindukia mipaka.
Jaji Stefan Bürgelin alisema kwenye hukumu yake kwamba dhamira ya mama huyo ni ya kulaaniwa na ushiriki wake kwenye kumdhalilisha mwanawe ulitokana na lengo la kuhakikisha kuwa mpenzi wake mpya hamuachi.
Baadaye, maslahi ya kifedha yaliingia kati, ambapo wawili hao walipata maelfu ya euro kwa kumchuuza kijana wao kwa wabakaji.
Wawili hao walikuwa ndio watuhumiwa wakuu wa mtandao wa wabakaji wanaopenda kufanya mapenzi na watoto wadogo uliokuwa ukifanya shughuli zake katika mji wa Staufen, kando kigodo ya Freiburg.