- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANAHABARI NA MKEWE WASHIKILIWA KWA MAUWAJI
Mahakama Kuu ya Mjini Nairobi nchini Kenya imeagiza kuendelea kuzuiwa kwa washukiwa wawili Jacque Maribe na mpenzi wake Joseph Irungu kwa mauaji ya mwanadada Monica Kimani, aliyepatikana ameuawa nyumbani kwake mwezi Septemba.
Viongozi wa Mashtaka, wamesema watamfungulia kesi ya mauaji Mwanabahari maarufu nchini humo Jacque Maribe na mpenzi wake Joseph Irungu ambaye ndio mshukiwa mkuu.
Jaji Jessi Lessit amesema wawili hao watazuiwa hadi siku ya Jumatatu wiki ijayo, na kuagiza kuwa Bi. Maribe afanyiwe uchunguzi wa kiakili katika Hospitali ya wagonjwa wa akili kabla ya kujibu mashtaka yanayomkabili.
Irungu naye ametakiwa kupewa huduma ya matibabu baada ya kupata jeraha la bega. Hata hivyo, viongozi wa mashtaka wanadai kuwa mshukiwa huyo alijipiga risasi mwenyewe wala hakushambuliwa.
Kiongozi wa Mashtaka Noordin Haji, ameagiza wawili hao kufunguliwa kesi ya mauaji kwa madai kuwa walishirikiana kumuua mwanadada huyo.