- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANAFUNZI ALIYEUWA WATU 10 TEXAS AFUNGULIWA MASHTAKA
TEXAS: Maafisa wa polisi katika mji wa Texas Ijumaa hii wamemfungulia mashtaka kijana mwenye umri ya miaka 17 kwa kosa la kuuwa katika shambulizi la bunduki lililouwa watu 10, wengi wao wakiwa wanafunzi, katika shule ya sekondari ya Santa Fe, Texas.
Watu wengine kumi walijeruhiwa katika shambulizi hilo, akiwemo afisa wa polisi anayelinda shule hiyo ambaye alikuwa mtu wa kwanza kukabiliana na mshukiwa huyo.
Wanafunzi wamesema mshambuliaji huyo aliyekuwa na silaha, ametambuliwa na vyombo vya usalama kama Dimitrios Pagourtzis, mwanafunzi wa shule ya sekondari ya awali, ambaye alishambulia shule hiyo kwa bunduki kabla ya saa mbili asubuhi.
Majina ya waliouwawa katika shambulizi hilo yanaendelea kutolewa, na kati yao ni mwalimu mbadala na mwanafunzi wa kigeni aliyekuwa katika programu ya shule hiyo ya kubadilishana wanafunzi.
Cynthia Tisdale, mwalimu, alikuwa kati ya wale waliouwawa Ijumaa asubuhi katika Shule ya Sekondari ya Santa Fe, familia yake imethibitisha.
Tisdale alikuwa katika ndoa yake na mumewe kwa miaka 40 na walikuwa tayari wana watoto watatu na wajukuu wanane, mpwa wao wa kike Leia Olinde amesema.
Sabika Sheikh, akiwa katika programu ya kubadilishana wanafunzi kutoka Pakistan, naye aliuwawa, Ubalozi wa Pakistan mjini Washington umethibitisha hilo.
Jumuiya ya Pakistan inayosimamia kuifanya Houston kuwa Bora Zaidi umesema katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Sabika alikuwa katika maandalizi ya kwenda Pakistan kwa ajili ya sikukuu ya Eid al-Fitr, mapumziko ya siku tatu ambayo yanaadhimisha kumalizika kwa mwezi wa Ramadhan katika dini ya Uislam.