Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:52 am

NEWS: MWANAFUNZI ABURUZWA MAHAKAMANI

Serengeti. Watu wawili akiwamo mwanafunzi wa Sekondari ya Mugumu Kurwa Daniel (19) na raia wa kawaida Paulo Marwa (30) wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Serengeti mkoa Mara wakidaiwa kuiba pikipiki.

Akiwasomea mashtaka hayo leo Agosti 2 mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Ismail Ngaile Mwendesha mashtaka wa Polisi Renatus Zakeo ameiambia mahakama kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Julai 27 mwaka huu.

Mwanafunzi Daniel yeye alikamatwa leo Agosti 2 akiwa shule, akasomewa mashtaka akiwa amevaa sare zake za shule na mkononi akiwa meshika madaftari yake.

Amesema waliiba pikipiki aina ya Toyo mali ya Benjamin Kiboge yenye thamani ya Sh2 milioni.

Washtakiwa wote wamekana mashitaka na wamepelekwa mahabusu hadi Agosti 10 mwaka huu itakapotajwa tena.