Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 10:58 pm

NEWS: MWALIMU AMPIGA MWANAFUNZI MPAKA KUMUUWA KWA TUHUMA ZA KUIBIWA

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mwalimu wa shule ya msingi ya Kibeta iliyoko katika Manispaa ya Bukoba mkoani kagera respicius patric aliyempiga na kumuua kikatili mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo spelius eradius baada kutumhumu kuwa ameiba mkoba wa mwalimu elieth gerald uliokuwa na vitu mbalimbali zikiwemo pesa tasilimi shilingi elfu sabini na tano na simu ya mkononi.

Image result for Kamanda Ullomi


kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Kamishina Msaidizi Mwandamizi Augustine Ullomi ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amefika katika shule hiyo na kukumbana na wakati mgumu baada ya wanafunzi kumpokea kwa nyimbo zilizokuwa ujumbe wenye maudhui ya kudai ya kudai haki yao.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika shule hiyo Kamanda Ullomi amekemea kitendo cha mwalimu huyo cha kumuua kikatili mwanafunzi huyo ambaye hakuwa na hatia yoyote kwa kuwa mkoba aliodai umedaiwa umeibiwa mwalimu alikuwa ameusahau kwenye pikipiki ilimsafirisha toka nyumbani kwake kuja shuleni na amesema jeshi hilo liwasaka popote pale walipo watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo kwa njia moja au nyingine ili liweze kuwachukulia hatua.

Wanafunzi hao walidai mwanafunzi mwenzao aliitwa na kuanza kuhojiwa kuhusu kupotea kwa pochi hiyo na akakana kuichukua, hali iliyosababisha kuanza kupigwa akitakiwa kuirejesha.

Walisema kuwa baadaye walitakiwa kuitafuta pochi hiyo mpaka chooni, lakini hawakuiona huku mwanafunzi huyo akiendelea kuadhibiwa.

Hata hivyo, ilielezwa na wanafunzi hao kuwa wakati mwanafunzi mwenzao akiendelea kupigwa, dereva bodaboda alifika shuleni hapo akimtafuta mwalimu aliyepoteza pochi na kumkabidhi pochi aliyokuwa ameisahau kwenye pikipiki yake.

Mashuhuda hao walisema kuwa baada ya pochi hiyo kupatikana, mmoja wa walimu aliagiza mwanafunzi huyo apatiwe juisi na bagia, chakula ambacho hakuweza kukila kutokana na maumivu.