- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWALIMU ABURUZWA MAHAKAMANI KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI WAKE
Arusha: Kesi inayomkabili Mwalimu wa shule ya Sekondari Adili iliyopo jiji la Arusha, Joel Mbaga(27), ya kumlawiti mwanafunzi wake wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 13, (jina linahifadhiwa) ,Shahidi Nambari moja wa kesi hiyo jana ameieleza mahakama kuwa, mwanafunzi huyu alianza kugoma kwenda shuleni kutokana na tukio hilo la kulawitiwa.
Shahidi huyo ambaye ni mama mzazi wa mwanafunzi huyo, amesema baada ya kugoma kurejea shule ndipo alieleza amekuwa akilawitiwa na mwalimu wake. Akiongozwa na wakili wa Serikali, Naomi Mollel mbele ya Hakimu mkazi wa Wilaya ya Arusha, Patricia Kisinda, shahidi huyo alisema baada ya kumbana kwa maswali mtoto wake, alimtaja mwalimu Joel Mbaga.