- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : MUUNGANO WA MAVETERANI ZIMBABWE WAITISHA MAANDAMANO DHIDI YA MUGABE
Muungano wa maveterani wa vita Zimbabwe waitisha maandamano dhidi ya Rais Mugabe
Muungano wa maveterani wa vita vya uhuru nchini Zimbabwe umetoa wito wa kufanyika maandamano dhidi ya Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo ili kumshinikiza ajiuzulu na kuachia madaraka ya nchi.
Mkuu wa Muungano wa Maveterani wa Vita nchini Zimbabwe ametaka kufanyika maandamano dhidi ya Mugabe haraka iwezekanavyo na kumshinikiza kiongozi huyo ajiuzulu.
Chris Mutsvangwa amesema leo kuwa, anawataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika maandamano ili kumshinikiza Mugabe aliyekaa madarakani kwa muda wa miaka 37 ajiuzulu na kuachia hatamu za uongozi wa nchi.
Wakati huo huo, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Harare mji mkuu wa Zimbabwe wameandamana dhidi ya Mugabe aliye na miaka 93 huku wakipiga nara dhidi ya kiongozi huyo wakimtaka aondoke madarakani. Viongozi wa chuo hicho kikuu cha mjini Harare wamesema kuwa, wameakhirisha mitihani iliyotazamiwa kufanywa chuoni hapo hadi wakati mwingine. Jeshi la Zimbabwe Jumatano tarehe 15 mwezi huu lilitangaza kuwa Mugabe na familia yake wapo katika kifungo cha nyumbani na kisha kumuondoa uongozini.
Jeshi la Zimbabwe lilichukua hatua hiyo kama radiamali kwa hatua ya siku kadhaa zilizopita iliyochukuliwa na Mugabe ya kumuuzulu aliyekuwa Makamu wake Emmerson Mnangagwa ili aweze kumrithisha nafasi hiyo mkewe Bi Grace Mugabe,Hivi sasa Mugabe anakabiliwa na mashinikizo ya kujiuzulu kutoka kila upande ingawa hadi sasa bado kiongozi huyo wa muda mrefu madarakani hajasalimu amri na kukubaliana na matakwa ya kujiuzulu.