- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MUSWADA WA SHERIA YA JIJI LA DODOMA KUWA MAKAO MAKUU YAIVA.
BUNGENI DOM: Serikali imewasilisha muswada wa sheria ya kulitangaza jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi wa mwaka 2018 unaopendekeza kutungwa sheria ili kutambua kisheria kuwa Dodoma ni makao makuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiwasilisha Muswada huo leo bungeni jijini Dodoma waziri wa Nchi ofisi ya Rais,tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo amesema chimbuko la hoja ya kutunga sheria hiyo ni kukosekana kwa sheria inayotambua na kuweka misingi ya uendelezaji wa Makao Makuu ya nchi.
Akitoa maoni ya kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na serikali za mitaa,mwenyekiti wa kamati hiyo Jasson Rweikiza amesema ni wakati mwafaka wa sheria ya Tamko la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi ikaanza kutumika mapema.
Wakichangia muswada huo wabunge wameunga mkono na kuiomba serikali kuharakisha ujenzi wa miundombinu.