- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MUSEVEN ATOA SH. 5MIL KWA KILA MFIWA KWENYE AJALI YA GARI UGADA
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa Shilingi za nchi hiyo Milioni 5 kwa kila Familia kuisadia katika shughuli za mazishi kufuatia vifo vya watu 22 baada ya ajali ya barabarani katika Wilaya ya Kiryandongo mwishoni mwa wiki iliyopita. Pia ametangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa,
Bendera zote nchini humo zinapepea nusu mlingoti kwa heshima ya watu hao. Ajali hiyo ilihusisha basi la abiria na Lori la mizigo.
Takriban watu 22 wakiwemo watoto watatu waliuwa kwenye ajali ya basia lililogonga tingatinga ambayo ilikuwa ikiendeshwa bila ya taa usiku kwa mujibu wa msemaji wa polisi Emilian Kayima ambaye aliongea na AFP.
Awali shirika la msalaba mwekundu lilisema kuwa jumla ya vifo ni 48 wakiwemo watoto 16.
Uganda ina kati ya rekodi mbaya zaidi za usalama wa barabara. Zaidi ya watu 9,500 waliuawa kwennye ajali za barabarani nchini humo kati ya mwaka 2015 na 2017 kwa mujibu wa takwimu rasmi