Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 3:48 am

NEWS: MULTICHOICE TALENT FACTORY MKOMBOZI KWA VIJANA.

DODOMA: Waziri wahabari, utamaduni, sanaa na michezo Dk Harison Mwakyembe amewataka wadau wa filamu nchini wasisite kushirikiana na serikali katika mambo mbalimbali hususan ya kisera, kanuni na hata sharia ili kuleta maendeleo ya kweli katika taifa letu.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo mei 30 wakati wa hafla ya uzinduziwa mradi wa Multichoice Talent Factory iliyofanyika jijini Dodoma

Aidha amesema pamoja na kukuza maslahi ya nchi pia itasaidia kuendeleza utamaduni na kuleta hadhi kwa jamii ya watanzania.

Mbali na hayo amesema Kwa upande wa sekta ya Filamu MultiChoice Tanzania kupitia DStv wamekuwa na mchango mkubwa na jitihada kubwa katika kuiinua tasnia hiyo hususan kwa kuongeza maudhui (contents) za ndani.

Hata hivyo amesema kuanzishwa kwaMultiChoice Talent Factory kutawezesha kupata wataalam waliobobea zaidi katika fani hiyo na hivyo kuongeza ubora wa kazi zetu za filamu na hivyo kuzifanya ziwe na soko kubwa ndani na nje ya nchi na kuwataka vijana kuchangamkia fursa hiyo.

Awali akizungumza mkurungezi Mkurugenzi wa MultiChoice Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi Maharage Chande amesema Multichaoice imeanzisha programu hiyo yenye lengo lakuibua vipaji hapa nchini katika maeneo ya filamu na kisha kuvipa mafunzo (kuvipika) ili viweze kushindana katika medani za kimataifa kwa manufaa ya kwao(hao wenye vipaji) na kwa taifa kwa ujumla.

Amesema katika karne ya sasa vijana wamekuwa mstari wa mbele katika uzalishaji wa maudhui ya filamu na muziki duniani kwa umahiri mkubwa na kuhakikisha kuwa kazi ambazo wanazinunua na kuziweka kwenye ving’amuzi vyao nyingi zitoke Afrika na ziwe za kiwango cha juu.

Licha ya hayo amesema wanaamini programu hiyo itasaidia vijana wa Kitanzania watafaidika kwa kupata mapato yatokanayo na kazi zao kutoka ndani na pia nje ya nchi kutokana na ubora wa kazi zao na kuongeza kuwa Kwani mafanikio ya watanzania watakaopata nafasi yanaendana pia na sera ya vijana na ajira, elimu pamoja na viwanda na biashara(Holywood).