- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MUGABE AGOMA KUHOJIWA NA KAMATI YA BUNGE LA ZIMBABWE
HARARE: Rais wa zamani wa Zimbabwe, Bw. Robert Mugabe kwa mara ya pili mfululizo amegoma kwenda bungeni ili kuhojiwa mbele ya kamati ya uchunguzi wa mapato ya Almasi juu ya upotevu wa kipande cha Almasi chenye thamani ya dola $15 Bilioni katika kipindi cha utawala wake.
Mugabe alitakiwa kwa mara ya kwanza kutokea mbele ya kamati tarehe 23 Mei 2018 saa 3 asubuhi na kutotokea kwake kulidhaniwa kuwa ni sababu ya uzee hivyo alishindwa kufika muda wa asubuhi wakadhani huenda akatokea mchana wake kitu ambacho hakikufanyika.
Kwa mara ya pili Mugabe alitakiwa kufika tarehe 28 Mei 2018 saa 7 mchana lakini pia ameshindwa kufika hivyo kama sheria inavyosema ataitwa mara ya 3 kabla vyombo vya dola havijapewa kazi ya kumfikisha Bungeni kwa nguvu.
Rais huyo aliyeongoza kwa muda mrefu hadi alipotolewa madarakani Novemba mwaka 2017, ametakiwa kufika Bungeni hapo tarehe 11 Juni, 2018 bila kukosa.
Mugabe, mwenye umri wa miaka 93, amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu mwaka wa 1980.
Alikuwa Waziri Mkuu hadi 1987 alipochukua usukani kama rais wa nchi hiyo. Utawala wake wa miaka 37 umeshutumiwa kwa ukandamizaji wa upinzani, ukiukaji wa sheria za uchaguzi, na kusababisha uchumi wa nchi kuanguka.
Alipokuwa kijana, Mugabe alikuwa mmakinifu na mzuri kabisa katika mchezo wa tenisi, kulingana na aliyekuwa mwalimu katika shule ya Wakatoliki alikosomea Mugabe. Ila, aliposhindwa katika mchezo huo, aliitupa raketi yake chini kwa hasira.
Mugabe amekiri kuwa hakuwa mzuri katika mchezo wa kandanda alipokuwa mdogo, ila kwa sasa, anapenda kuutazama mchezo huo.
Yeye ni shabiki wa klabu za Chelsea na Barcelona.
Mwanasiasa huyo alipata umaarufu mkubwa kwa mara ya kwanza pale alipoongoza vita vya msituni dhidi ya wakoloni walioitawala Zimbabwe, wakati huo ikijulikana kama Rhodesia.
Mugabe alikamatwa na kufungwa jela kwa kipindi cha miaka kumi kufuatia hotuba aliyoitoa manamo mwaka wa 1964, iliyowagadhabisha wakoloni ambao waliitaja kuwa ya uchochezi.
Aliachiliwa kutoka jela mnamo mwaka wa 1974 na kuingia kwenye siasa za kushinikiza Waingereza kusitisha utawala wake kwa Rhodesia.
Baadaye Mugabe alitorokea nchi jirani ya Msumbiji na kurudi Rhodesia mnamo mwaka wa 1979.