- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTU MMOJA AOA WAKE WA WILI KWA MPIGO
Mwanaume mmoja jina Tom Mako kutoka jamii ya kimasai mkazi wa eneo la Kajiado nchini Kenya ameshangaza umma baada ya kufunga ndoa na wanawake wawili kwa mpigo.
Tom maarufu kama Junior, mwenye umri wa miaka 27, alifanya sherehe hiyo ya harusi Jumanne wiki hii iliyohudhuriwa na ndugu jamaa na Marafiki lukuki.
Mako anatokea kwenye familia ambayo ndoa za mitala ni jambo la kawaida
Mako aliwaoa Elizabeth Silamoi, 25, na Joyce Tikoyian, 23 Wote wawili ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Kenya Assemblies of God mjini Kitengela, si mbali sana na eneo Kisaju anakoishi Tom.
"Nataka kuliweka sawa hili, harusi yangu ilikuwa ya kimila na haikuwa na mahusiano yoyote na kanisa. Kuna watu wanatuma habari za kupotosha mitandaoni kuwa ndoa yangu ilisimamiwa na wachungaji," Mako, ambaye ni mfanyabiashara, amenukuliwa na gazeti la kibinafsi la Star la nchini Kenya.