- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : MTOTO WA MIEZI NANE NI MMOJA YA WALIOUAWA KIKATILI NA JESHI LA ISREAL
Mtoto mwenye umri wa miezi minane tu ni mmoja wa wahanga wa ukatili wa hivi punde wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Wizara ya Afya ya Gaza imetangaza kuwa, mtoto huyo kwa jina Leila al-Ghandour amefariki dunia baada ya kuvuta gesi ya mabomu ya kutoa machozi yaliyovurumishwa na jeshi la utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza siku ya Jumatatu.
Picha za kuatua moyo zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha familia ya binti huyo mdogo wakiwemo wazazi wake wakiukumbatia mwili wa mtoto huyo, huku wakibubujikwa na machozi.
Watoto wanane ni miongoni mwa makumi ya watu waliouawa katika mauaji hayo ya umati yaliyofanywa na jeshi katili la Israel, dhidi ya Wapalestina wa Gaza, waliokuwa wakiandamana kulalamikia kughusubiwa ardhi zao.
Hii ni katia hali ambayo, Ikulu ya Marekani White House ilijitokeza hadharani hivi karibuni kuutetea utawala huo wa Kizayuni kwa kuwaua shahidi Wapalestina zaidi ya 60 waliokuwa wakishiriki maandamano katika Ukanda wa Gaza siku ya Jumatatu, huku ikiwalaumu Wapalestina hao kwa mauaji dhidi yao.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina tayari imemuita nyumbani balozi wake wa Washington, Husam Zomlot ambaye anatazamiwa kuondoka Marekani leo Jumatano