Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 3:47 am

NEWS: MTOTO WA LOWASSA AJITOSA UBUNGE MONDULI

Arusha: Mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani , Edward Lowassa, Fred Lowassa, jana amechukuliwa fomu na wanachama wa chadema kuwania ubunge Jimbo la Monduli, kupitia chama hicho

Lakini kwa upande wa Fred hakupatikana kuzungumzia suala hilo, dalili za kujitosa kwenye uchaguzi, zilianza kuonekana baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Julius Kalanga, kujiuzulu na kujivua uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya kujiuzulu kwa Kalanga, baadhi ya vijana wa Chadema akiwamo Diwani wa Sombetini, Ally Bananga, waliandika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa dawa yake ni kumpelekea Fred apambane naye kwenye uchaguzi mdogo.

“Huyu ndiye wa kwenda kumzima Kalanga, uchaguzi mdogo ukiitishwa nitakishawishi chama changu twende na Fred Lowassa, kampeni meneja nakamata mwenyewe mzee baba,” ilisema sehemu ya ujumbe kwenye ukurasa wa Instagram wa Bananga, ambaye ni mmoja wa vijana wenye ushawishi mkubwa ndani ya Chadema.

Uchaguzi wa jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Septemba 16.

Alipohojiwa Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, kujua juu ya watia nia wengine alitaja watia nia wengine kuwa ni Cecy Ndosi ambaye ni Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Arusha na Diwani wa Viti Maalumu, Jimbo la Monduli na Yonas Laizer ambaye ni Diwani wa Kata ya Lepurko.

Golugwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, alisema wengine waliochukua fomu ni Erick Ngwijo na Lelubu Kivuyo.

Alisema baada ya watia nia hao kurejesha fomu hizo jana, kikao cha kupiga kura ya maoni kitafanyika Agosti 11 kabla ya Kamati ya Utendaji ya Wilaya kukaa na kutoa mapendekezo yake kisha kupelekwa Kamati Kuu ya chama hicho.

“Baada ya hapa Monduli, Jumamosi tuna mkutano wa wilaya wa kura ya maoni ambao utafanyika Kata ya Migungani, halafu siku hiyo hiyo Kamati ya Utendaji ya Wilaya itakaa na kuweka mapendekezo yake na yatachuliwa na ofisi yangu ya kanda na kupeleka makao makuu kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama kwa maamuzi,” alisema