- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTATIRO AMEWATAKA VIJANA WALIOBAKI UPINZANI KUJIUNGA CCM
Dar es salaam: Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa chama cha wananchi CUF taifa, Julius Mtatiro amewataka vijana kuvikimbia vyama vyao vya upinzani hapa nchini nakusema kuwa ni mali za watu fulani.
Akiongea leo Sept. 7, 2018 wakati alipokuwa akimnadi mgombea wa jimbo la Ukonga kwa tiketi ya CCM ndugu Mwita Waitara katika kampeni zilizofanyika eneo la Pugu Kajiungeni na kuwataka vijana kuachana na vyama vya upinzani na kujiunga CCM ambapo ndicho chama kinachopigania maendeleo ya Watanzania kwa ujumla.
"Msishangae kabisa vijana wengi wenye akili zao timamu wakaendelea kuondoka vyama vya upinzani wakahamia Chama Cha Mapinduzi ni maamuzi tu, vyama vya upinzani vinawachukulia vijana for granted, mimi nimekaa upinzani kwa miaka 10 nimefanya juhudi kubwa sana kurekebisha makosa makubwa ambayo yamekuwa yakifanywa na vyama vya upinzani lakini mwisho wa siku vyama vile vimeshikiliwa na watu" β Amesema Julius Mtatiro.
Mtatiro amewasihi wananchi wa jimbo la Ukonga kumchagua Mwita Waitara kuwa mbunge wao kwa maendeleo ya jimboni hapo huku akielezea historia ya uongozi aliyonayo mgombea huyo tangu alipokuwa rais wa wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam na harakati za kupigania haki ya kupewa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchi nzima.
β"Mkimpata Waitara kuwa mbunge wa Ukonga na mara hii akitokea kwenye chama kinachoongoza dola akiungana na viongozi wa mkoa, wakuu wa wilaya, mawaziri na akiungana na chuma John Pombe Magufuli mambo ya Ukonga yatakwenda mbio sana" - Mtatiro.