- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTANZANIA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KENYA
Raia wa mmoja wa Tanzania jina Msafiri Mussa '43' ni miongoni mwa raia wa nchi za nje 18 ambao wanazuiliwa nchini Kenya baada ya kukamatwa akiwa ameficha madawa ya kulevya kwenye njia yake ya kwenda haja kubwa (rektamu).
Walikuwa safarini kuelekea China na India walipokamatwa Alhamisi usiku katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Mtanzania huyo ambaye ametambuliwa na idara ya uchunguzi wa jinai nchini Kenya alitoa tembe 47 za dawa za kulevya mara ya kwanza.
Aliwekwa chini ya uangalizi ambapo baadaye alitoa tembe nyingine 69.
Polisi hawajasema raia wa mataifa hayo mengine ni kina nani.
"Wachunguzi wa jinai wamewasilisha maombi katika mahakama ya JKIA kumzuilia zaidi ili kuwawezesha kukamilisha uchunguzi. Washukiwa bado wanaendelea kuangaliwa kwa makini," idara ya uchunguzi wa jinai Kenya imesema kupitia ukurasa wake wa Twitter.