- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSIGWA NA RIDHIWANI KIKWETE WATUNISHIANA MISULI BUNGENI
Dodoma: Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa na Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete leo Jumatano, wamerushiana maneno bungeni kila mmoja akionyesha unguli wake katika kutunga sheria.
Ugomvi huo umetokea leo katika Bunge lilipoketi kama kamati chini ya mwenyekiti wa Bunge, Najma Murtaza Giga kupitia vifungu vya muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa 2017
Mabishano yao yalikuwa kama hivi:
Ridhiwan: Mwenyekiti Taarifa
Msigwa: Hatutoagi taarifa kwenye kuchangia
Ridhiwani: Leo ndio unapewa taarifa hapa leo. Wanataka kutuyumibisha bwana. Hatuwezi kuyumbishwa bwana sisi tunatengeneza sheria.
Msigwa: Hata mimi natengeneza sheria
Ridhiwani Hakuna namna hiyo Msigwa bwana. Hatuwezi kutunga sheria ambazo ziko biased (zina pendelea)
Mwenyekiti wa Bunge: Waheshimiwa wabunge. Naomba mkae nyinyi nyote wawili Naomba mkae wote wawili. Mheshimiwa AG Tuendelee.
Ridhiwan: Sie tumesoma sheria bwana
Mwenyekiti wa Bunge: Mheshimiwa Stella Manyanya (Naibu Waziri wa Elimu)
Stella Manyanya: Kwanza nataka kumuambia Bwana Msigwa . Si vyema kutumia vibaya kumtaja mheshimiwa Rais kwa mambo ambayo sio lazima sana. Kwa mfano kumwambia alimuondoa mbunge”