- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSHAURI WA PAPA ATAKA MJADALA UNYANYASAJI WA KINGONO
Mshauri wa juu wa Papa Francis, Kadinali Reinhard Marx amelitahadharisha Kanisa Katoliki kuwa liko hatarini kuingiliwa zaidi na mamlaka ya polisi na serikali ikiwa halitashughulikia kashfa za unyanyasaji wa kingono kwa mapadri kwa kufanya mageuzi makubwa.
Kardinali Reinhard Marx ametoa wito wa kuwa na "mjadala wa wazi" ndani ya Kanisa Katoliki kuhusu ubasha, matumizi mabaya ya mamlaka na "useja na mafunzo ya upadri" kama sehemu ya muitikio kwa kadhia za ukiukaji wa kingono.
"Ikiwa hakuna hatua za kurekebisha zitakazochukuliwa na Kanisa -- na tunafanyia kazi hilo, tunapaswa kulifanyia kazi ---serikali haitakuwa na njia nyingine zaidi ya kuigilia," alisema Marx siku ya Ijumaa, akizungumzia uchunguzi unaoendelea dhidi ya viongozi wa Kanisaa katika mataifa kama Chile, Marekani na kwingineko.
Marx, mmoja kati ya washauri tisa wa kipadri wa papa Francis, alitoa matamshi yake katika uzinduzi wa shahada ya uzamili kuhusu ulinzi wa watoto katika chuo kikuu cha kichungaji cha Gregorian mjini Roma, ambako majesuti wanafundishwa. Uzinduzi wa kozi hiyo umekuja wakati Vatican imewakusanya mapadri zaidi ya 250 kujadili namna ya kuboresha uchungaji kwa vijana.