Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:45 pm

NEWS: MPINZANI WA KAGAME INGABIRE ASALIMU AMRI BAADA YA KUTOKA KIFUNGONI

Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda aliyetoka gerezani kwa msamaha wa Rais Kagame Victoire Ingabire Umuhoza ameseema kwasasa yuko tayari kusaidaia maendeleo ya nchi ya Rwanda baada ya kuachiliwa huru.

"Nina furaha kwa hatua iliyochukuliwa na rais na sasa nitarejea kuendelea na maisha kama kawaida na kusaidia maendeleo ya nchi,"amesema Ingabire, akinukuliwa na gazeti la The New Times la Rwanda.

Ingabire, ni miongoni mwa wafungwa zaidi ya 2000 walioachiliwa huru kwa msamaha wa rais Paul Kagame. Walihukumiwa kwa nyakati tofauti na walikuwa wakitumikia vifungo vyao katika gereza la Nyarugenge.

Ingabire ni kiongozi wa chama cha upinzani cha United Democratic Forces of Rwanda (FDU-Inkingi) na alihukumiwa kwenda jela kifungo cha miaka 15, miaka minane iliyopita.

Tangu wakati huo ulimwengu umekuwa ukipaza sauti kuachiliwa kwake na hatua ya serikali ya Rwanda kumuachilia huru inatajwa kuwa hatua muhimu kuchukuliwa na utawala wa rais Paul Kagame ambaye anaongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa muhula wa tatu sasa.

Mwanaharakati mwingine aliyeachiliwa huru ni mwanamuzi Kizito Mihigo ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kukutwa na hatia ya kuratibu njama za mauaji ya rais Paul Kagame.