Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:48 pm

NEWS: MOROCCO YAZINDUA TRENI YENYE KASI ZAIDI BARANI AFRIKA

Taifa la Morocco limefanikiwa kuzindua treni inayokwenda kwa kasi zaidi barani Afrika - itakayopunguza nusu ya muda uliokuwa unaotumika kusafiri katika miji ya kibiashara na miji ya kiviwanda (Casablanca na Tangi)

katika safari ya uzinduzi Mfalme Mohammed VI na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron waliipanda treni hiyo kutoka mji wa Tangier hadi katika mji mkuu Rabat.

Treni hiyo imepangiwa kwamba itakwenda kwa kasi ya 320km kwa saa
Itakapunguza kwa zaidi ya nusu muda unaotumika kusafiri 200km kutoka mji wa Casablanca hadi Tangi kuwa safari ya saa mbili.

Inakwenda kwa kasi ya mara mbili zaidi kuliko treni ya mwendo kasi ya Afrika kusini inayouunganisha uwanja wa kimataifa wa ndege Johannesburg hadi katika mji wa kibiashara wa Sandton
Inagharimu 22.9 billion dirhams ($2.4bn; £1.8bn), kwa mujibu wa shirika la habari la kitaifa MAP
Ilichukua miaka saba kuijenga reli ya treni hiyo.