- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MNYIKA AWAJIBU WANAOSEMA ANAHAMIA CCM KWA STAILI HII
Dar es salaam: Mbunge wa Kibamba (CHADEMA) na Naibu Katibu Mkuu (Bara) CHADEMA John Mnyika amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwa siku kadhaa baada ya kuhusishwa kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM sasa leo amejibu tuhuma hizo kwa kuonesha kuunga mkona wabunge wawili wa CHADEMA Peter lijuakali na Susan Kiwanga baada ya mahakama ya hakimu mkazi Mororogoro kuwanyima dhamana wabunge hao "Nasimama na wabunge wetu wawili; Ndugu Peter Lijuakali na Susan Kiwanga, Madiwani wetu wawili na wanachama wetu 34 ambao kwa mara ya pili sasa bado wanakataliwa kupewa dhamana" alisema Mnyika
Akiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram Mnyika alisema kuwa watu wakumbukwe kuwa wabunge hao walikamatwa toka Novemba 26 mpaka sasa wananyimwa haki yao ya msingi ya kupata dhamana. Ninaheshimu mhimili wa Mahakama; lakini kwa yaliyowahi kwisha tokea na mifano lukuki inasukuma hitaji la sauti zetu. Kumeshakuwa na njama ovu nyingi dhidi yetu wapinzani hasa ktk suala zima la utoaji wa haki ya msingi ya dhamana-inahitaji kupazwa sauti zetu na kuunganisha nguvu kukemea hili.
Tuungane ktk hili na madhila mengine mengi ya uvunjifu wa haki, demokrasia na usawa ktk kuendesha siasa nchini. Tunahitaji siasa safi ili tuweze kupiga hatua kimaendeleo kama alivyotuasa Baba yetu, Mwl. Julius Nyerere.
Aluta continua! alimalizia Mnyika
Wabunge wahao walikosa dhamana jana baada ya kuibuka kwa hoja za kisheria Upande wa mashtaka na ule wa utetezi unavutana kuhusu hati ya kiapo ya kupinga dhamana iliyowasilishwa mahakamani hapo.
Kutokana na mvutano wa kisheria, hakimu Ivan Msack ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano Desemba 6,2017 ili kutoa fursa kwa pande zote mbili kujibu hoja kuhusu hati hiyo kwahiyo washtakiwa hao wamerejeshwa rumande mpaka hapo kesho.
Wabunge hao wanakabiliwa na mashtaka nane likiwamo la kuchoma moto ofisi ya Kata ya Sofi iliyopo wilayani Malinyi.
Washtakiwa wanatetewa na mawakili Peter Kibatala, Ignas Punge, Fredrick Kiwelo na Bartholomew Tarimo.
Upande wa mashtaka unawakilishwa na mawakili wa Serikali, Edga Bantulaki na Sunday Hyera.