- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MNYIKA AMTAKA RAIS MAGUFULI KURUDISHA MCHAKATO KATIBA MPYA
Dar es salaam: Mbunge wa Jimbo la Kibamba (CHADEMA), John Mnyika amemuomba Rais Dkt. John Magufuli kulishughulikia marekebisho ya Katiba kabla ya kuelekea katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.
Hayo amezungumza na waandishi wa habari leo Agosti 08, 2018 wakati wa majadiliano kuhusu mabadiliko ya kikatiba na kisheria kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ili kusudi pawepo na chaguzi huru na haki.
Mnyika amesema ili kuepusha nchi isiingie kwenye matatizo ya kisiasa kuelekea mwaka 2020, "ushauri wangu na rai yangu kwamba Rais Magufuli ni vyema angekubaliana na makubaliano ambayo Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliyaridhia kuhusiana na marekebisho ya Katiba. Kwa mazingira yanayoonekana kwenye chaguzi ndogo hadi hivi sasa ni wazi kabisa kuna haja ya kufanyiwa marekebisho ya katiba ili kusudi ipatikane tume iliyokuwa huru", amesema Mnyika.
Mbali na hilo, Mnyika amedai bila ya kufanyika mabadiliko hayo bado kutakuwepo na tatizo kubwa ndani ya Tume ya uchaguzi kwa kushindwa kufanya kazi zao kwa uhuru.
Mnamo Novemba 20, 2016 Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) iliitaka serikali ya inayoongozwa na Rais Magufuli ifanye mabadiliko ya msingi katika Katiba kabla ya kuingia kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao wa Rais na Wabunge wa mwaka 2020.
Ambapo ilidai endapo mchakato huo wa kupata katiba mpya utafanyika basi itamwezesha Rais Magufuli kuacha kumbukumbu itakayomfanya akumbukwe wakati wote hata pale muda wake wa kuongoza utakapo kuwa umemalizika