Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:37 am

NEWS: MNADA MKUBWA WA VIWANJA KUFANYIKA DOM

DODOMA: Halmashauri ya Jiji la Dodoma linakusudia kuuza viwanja maalum 14 kwa njia ya mnada na mnada huo utafanyika siku ya Alhamisi 10 januari mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa,Mkuu wa Idara ya Ardhi,Mipango Miji na Maliasili katika Jiji la Dodoma Joseph Mafuru alisema kuwa viwanja hivyo ni kwa ajili ya biashara kwa wawekezaji ambao watakuwa wanahitaji kupata mahitaji muhimu ya viwanja hivyo.

Amesema kuwa viwanja ambavyo vinatarajiwa kuuzwa kwa njia ya Mnada vitakuwa na matumizi ya Vituo vya kuuza mafuta, kituo cha afya na matumizi mengine maalumu kwa wale ambao watahitaji kuwekeza.

Katika hatua nyingine Mafuru alisema kuwa wale watakakao kuwa tayari kununua viwanja hivyo watatakiwa kufika katika ofisi za Jiji kwa zamani zilikuwa ofisi za manispaa tarehe 8 Januari mwaka huu kwa ajili ya kwenda kuvikagua viwanja hivyo kabla ya mnada.

Amesema kuwa siku yam nada wanunuzi watatakiwa kulipa asilimia 25 ya manunuzi na baadaye watalazimika kulipa na kumalizia fedha yote ndani ya siku 14 kwa maana ya wiki mbili.

“ Mnunuzi atalazimika kulipia asilimia 25 ya mauzo ya kiwanja na baadaye ndani ya wiki mbili atalazimika kuwa amemaliza kulipia fedha yote, hii ni kutokana na kuhakikisha kila aliyenunua kiwanja anakuwa mnunuzi halisi na siyo dalali.

“Kumekuwepo na taratibu za madalali kuvamia minada na kununua viwanja au bidhaa mbalimbali ambazo zinauzwa katika mnada na badala yake madalali wamekuwa wakitafuta wateja wengine jambo ambalo linasababisha kuwepo na mlolongo mkubwa , kutokana na hali hiyo sasa tutahakikisha tunawathibiti nadalali katika kufanya biashara ya jinsi hiyo”Amesema Mafuru.