- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKUU WA MAJESHI ASEMA WAKO HATUA ZA MWISHO KUKIINUA MV NYERERE
Dar es Salaam: Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo amesema kwamba wako katika hatua za mwisho mwisho za kukisimamisha kivuko cha Mv Nyerere kilichozama Septemba 20,2018 katika Kijiji cha Ukara wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza.
Akizungumza leo Septemba 25, 2018, Mabeyo amesema wanahakikisha kivuko hicho kinasimama katika hali yake ya kawaida baada ya kufanikiwa kukigeuza na kuwa ubavu.
"Pia tunaendelea na uokozi wa baadhi ya miili ambayo huenda ilikuwa imelaliwa na mizigo hadi pale tutakapojihakikishia kuwa tumeimaliza yote ndani ya kivuko hiki" amesema Mabeyo.
Idadi ya Miili ya watu waliokufa katika ajali hiyo imefikia 227 baada ya mwili wa mtoto mmoja kuopolewa asubuhi ya leo katika Ziwa Victoria