Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 6:26 am

NEWS : MKUU WA JESHI LA POLISI UGANDA AWATAKA RAIA KUWAPIGA MAWE POLISI WANAPOKAMATWA BILA KUJITAMBULISHA

Mkuu wa polisi nchini Uganda ameamrisha wananchi kuwakamata au kuwapiga mawe maafisa wa polisi wasiojitambulisha wanapokuja kuwakamata washukiwa hata kama wamebeba bunduki.

Raia wa Uganda wanadai kwamba wanashindwa kuwatambua wanaowateka nyara jamaa zao, kwani wana tabia sawa na za maafisa wa polisi, wanao wakamata raia bila ya kujitambulisha, wala kuvalia sare za kikazi.

Polisi wa Uganda wakifanya mazoezi.

"Afisa wa polisi anapewa mafunzo jinsi ya kumkamata mshukiwa. Anastahili kujitambulisha na kumweleza mshukiwa sababu za kumkamta kabla ya kumkata. Kama hafanyi hivyo, raia wawakamate au wawapige mawe," amesema Kamanda Okoth Ochola.

Karibu kila siku, matukio ya mtu kutekwa nyara, hasa wasichana na akina mama yamekuwa yakiripotiwa nchini Uganda.

Image result for UGANDA ARREST CITIZEN

Utekaji nyara pia umesambaa na kuwalenga watoto wadogo, chini ya miaka 5 licha ya maafisa wa polisi na jeshi kuingilia kati kukabiliana na watekaji nyara.

Mkuu wa polisi anahusisha utekaji nyara huo na makundi ya kigaidi, na amesema : "Baadhi ya washukiwa ambao tumewakamata wana uhusiano na makundi ya kigaidi lakini sitayataja kwa wakati huu kwa sababu bado tunafanya uchunguzi. Tutakapokamilisha uchunguzi wetu, tutawaeleza."

Related image

Visa vya utekaji nyara vimekuwa vikiendelea nchini Uganda kwa mda wa takriban mwaka mmjoa sasa. watekaji nyara hudai mamilioni ya pesa kama kikombozi, na hata baada ya kulipwa pesa wanazotaka, huwaua wale waliowateka nyara.