Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 7:34 am

NEWS: MKURUGEZI BAHI AWATAKA WANAWAKE KUFANYAKAZI KWA BIDII.

DODOMA: Mkurugezi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Rachel Chuwa amelitaka jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuboresha Maisha ya wanawake na kupunguza utegemezi ndani ya familia.

Ameyasema hayo Leo mjini hapa wakati wa akizindua jukwaa la uwezeshaji kiuchumi wa wanawake wilaya ya Bahi.

Chuwa amesema ili kufikia uchumi wa kati na viwanda ni wajibu wa jukwaa hilo kutumia fursa zilizopo katika nyanga za kimaendeleo.


Mbali na hayo amesema lengo La jukwaa hilo ni kuwezesha wanawake kushiriki katika Nyanja mbalimbali ya kijamiina kiuchumi,kuwasaidia kuongeza uelewa wa wanawake,upatikanaji wa wa mitaji , masoko,kujua sheria mbalimbali za nchi na kupata uelewa juu ya fursa zilizopo na kuongeza kasi ya kushirikikatika masuala ya mipango ya maendeleo.

Aidha ameongeza kuwalengojingine ni kutoa maamuzi na kushiriki nafasi za uongozi na kudai kuwa mwanamke akisha tambua haki zake katika jamii masuala ya unyanyasaji kinjisia yatapungua ama kuisha kabisa.

Moja ya mwanamke katika jukwaa hilo BlandinaMagawa Amesema jukwaa hilo litawasaidia kuwainua wanawake kiuchumi na kuwatoa katika imani potofuya kuwa wanawake hawezi mpaka awezeshwe .

Pia amesema ili kufikia uchumi wa kati na wa viwanda ni wakati sasa wa wanawake kuamka na kuzitumia fursa zilizopo katika kuleta maendeleo chanya na kuondoka utegemezi katika jamii.

Kauli mbiu ya jukwaa hilo ni Bahi yetu, viwanda vyetu wanawake tuungane kufikia uchumi waviwanda.