- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKURUGENZI KAMPUNI YA MADINI YA BULYANHULU ABURUZWA MAHAKAMANI
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni za Madini za Bulyanhulu na North Mara,na Pangea (Pangea Minerals Limited), Asa Mwaipopo (55), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne akikabiliwa na mashtaka yapatayo tisa yakiwamo utakatishaji fedha, Kugushi nyaraka na kujipatia Dola za Marekani 840,000.
Akisomewa mashtaka hayo leo Oktoba 23, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na mawakili wa serikali Faraja Nchimbi na Jacqline Nyantori, wamedai mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda mashtaka hayo Aprili 11 mwaka 2008 na Juni 30 mwaka 2017.
Mshtakiwa huyo pia anadaiwa kutenda makosa ya kula njama, kuongoza uhalifu wa kupangwa, kughushi, ukwepaji wa kodi na utakatishaji wa fedha.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, upande wa mashtaka ulidai upelelezi bado haujakamlikika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 31, mwaka huu ambapo upande wa utetezi umeomba upelelezi uharakishwe.