Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:48 am

NEWS: MKOA WA NJOMBE TISHIO KWA MAAMBUKIZI YA VVU

DODOMA: Serikali imetangaza kuanzisha mpango maalumu wa kuvamia Mkoa wa Njombe ili kudhibiti maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo yameendeleza kuungamiza mkoa huo kwa kinara kwa na asilimia 14.8.

Hatua hiyo imekuja baada ya kubaini tatizo linalochangia uendelevu wa maambukizi hayo ni baadhi ya mila za wakazi wa mkoa huo ikiwamo utakasaji.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama wakati akifungua mafunzo maalumu kwa Kamati ya Bunge ya Ukimwi leo mjini hapa.

Aidha Amesema baadhi ya mila za makabila ya mkoa huo ni kurithi wanawake pindi mwanaume anapofariki (utakasaji) hali inayochangia uendelevu wa VVU.

Amesema mkakati huo utaendelea katika mkoa wa Iringa ambao una asilimia 9.1 na Mbeya ambao ni wa tatu kwa kuwa na asilimia 9.0.

Ameongeza kuwa upatikanaji wa dawa hizo kwa sasa ni asilimia 60 hivyo ununuzi wa Ceptrine utasadia kupunguza maambukizi mapya ya Kifua Kikuu (TB) kwa kuwa wagonjwa wa VVU mara nyingi hupatwa na TB.

Hata hivyo akiwasilisha mada kuhusu hali ya Ukimwi nchini, Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Jerome Kamwela amesema Mwaka 2013 maambukizi mapya yalikuwa 72,000, mwaka 2014 maambukizi mapya 69,603 na mwaka 2015 maambukizi mapya 48,000.

Pia amesema wanaume wanaoongoza kufa kutokana na kukaidi kuchukua hatua pindi wanapotambua kuwa wana VVU.