- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : MKE WA RAIS MUGABE AKIMBIA NA KUTOKOMEA NCHINI NAMIBIA
MBUNGE wa upinzani nchini Zimbabwe, Eddie Cross, ameiambia BBC kwamba anaamini mke wa Rais Mugabe, Grace, ametorokea Namibia.
Mwanasiasa huyo wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) amesema anafahamu kwamba Grace aliruhusiwa kuondoka nchini humo usiku wa kuamkia leo na jeshi
Ameongeza kwamba alikuwa hana kwengine kwa kwenda kutafuta hifadhi baada ya kudaiwa kumdhalilisha mwanamitindo Afrika Kusini, jambo lililomaanisha kwamba hawezi kuwa salama huko.Hata hivyo, taarifa hizi hazijathibitishwa na jeshi.Nick Mangwana, mwakilishi wa chama tawala cha Zanu-PF nchini Uingereza ameambia BBC kwamba mwenyewe pia amepokea taarifa kwamba Grace hayupo tena nchini Zimbabwe.
Lakini Mangwana amesema katika siasa za Zanu-PF, Bi Mugabe ni mtu wa chini sana na hana usemi wowote.Amesema ana mamlaka tu kwa sababu ya kuwa ni mke wa Rais Mugabe.“Alichukua wadhifa wa juu kuliko ule anaostahiki kuwa nao,” amesema.
CHANZO: BBC SWAHILI