- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKANWA ANG'ARA UNYEKITI WA CCM MKOA WA DODOMA.
DODOMA: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa ameahidi kufanya kazi kwa uadilifu,bila ya kujali udini,ukabila kama njia moja wapo ya kulipa idadi ya kura alizopata katika uchaguzi wa CCM ngazi ya mkoa.
Katika uchaguzi huo uliofanyika jana Mkanwa alipata kura 1025 kati ya kura halali 1110 zilizopigwa.
Akitoa neno la shukrani mara baada ya kutangazwa mshindi na msimamizi wa Uchaguzi huo SUBIRA MGALU, MKANWA amewashukuru wajumbe kwa kumuamini na kuahidi kufanya kazi kwa kufuata Katiba ya CCM.
Aidha mkutano huo umemchagua Ismail Jama kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa(NEC)kupitia mkoa huo na wajumbe wawili kutoka kila wilaya kwa ajili ya kuwakilisha katika halmashauri kuu ya mkoa.
Wakati huo huo Jumuiya ya umoja wa Vijana ya CCM mkoa wa Dodoma imeahidi kusimama imara katika kuwaunganisha vijana na kukisaidia chama mkoa ili kiendelee kutembea kifua mbele katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020.
Akizugumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake mwenyekiti wa umoja huo mkoa BILLY CHIDABWA amesema wanajua wao kama jumuiya wana mchango mkubwa katika kufanikisha ushindi wa Chama hivyo jukumu hilo wanalibeba kwa uzito wa pekee.
Aidha amesema UVCCM mkoa wa Dodoma ipo ili kuendana na hali ya leo ilivyo na inayoendana na juhudi za rais JOHN MAGUFULI ambaye ni mwenyekiti wa Chama hivyo watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha dhamira ya rais inafanikiwa.
CHIDABWA ametoa wito kwa wanachama wa umoja huo kuacha kufanya kazi kwa mazoea ,waache kufanya siasa za matukio bali waitumikie UVCCM wakati wote ili matunda yatakayopatikana iwe msaada kwa Chama na umoja huo kwa ujumla.