Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:52 pm

NEWS: MISS TANZANIA AENDELEA KUSOTA MAHABUSU

Dar es Salaam: Kesi inayomkabili Miss Tanzania wa mwaka 1996 Shose Sinare ya uhujumu uchumi pamoja na wezake watatu akiwamo mwenyekiti wa kampuni inayoshughulika na Uwekezaji wa Mitaji na Dhamana (Egma) Harry Kitilya na wengine ambao ni Pamoja na Kitilya aliyewahi kuwa kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mwengine ni aliyekuwa ofisa wa Benki ya Stanbic, Sioi ambaye aliyekuwa anafanya kazi bank moja na Miss Tanzania huyo.

Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali, Patrick Mwita ameieleza mahakama Jana Ijumaa Novemba 9, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Mwita amedai wanawasiliana na wachunguzi ili wajue upelelezi umefikia wapi.

Baada ya wakili, Mwita kueleza hayo, Hakimu Shaidi ameiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 16, 2018 ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekwisha kamilika ama la.

Washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550 kwa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.

Wanadaiwa Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani milioni sita, wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.

Washitakiwa hao wanadaiwa kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani milioni sita katika akaunti tofauti tofauti za benki.