Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:46 am

NEWS: MIMBA KWA WANAFUNZI BADO NI TATIZO NCHINI.

DODOMA: Mimba za utotoni kwa wanafunzi imeonekana ni changamoto kubwa ambayo inachangia wasichana wengi kukatisha masomo na kusababisha kudumaza kiwango cha ufaulu nchini.

Hayo yamesemwa na mwezeshaji Geofrey Chambua kutoka mtandao wa TGNP wakati wa mkutano wa watekelezaji wakuu wa sera mbalimbali uliofanyika mjini hapa.

Hata hivyo amesema Miongoni mwa changamoto zingine ni pamoja na umbali kwa wananfunzi na mazingira duni ya shule na kuongeza kuwa upofu wa kijinsia katika utamaduni na utatuzi bado ni changamoto.

Moja ya wadau Tatu Maleta kutoka Morogoro amesema vishawishi na ukosefu wa vyumba vya falaga kwa wanafunzi wa kike bado ni changomoto kubwa ambayo inachangia kushindwa kijisitli kipindi cha hedhi.

‘’Utakuta mwanafunzi akiwa kwenye hedhi kubadilisha nguo za ndani mpaka aende nyumban hii inachangia kuchelewa masomo,’’amesema Maleta.

‘’Madereva bodaboda wanawashawishi nitakupa ‘lift’ msaada kila siku nitakuwa nakurudisha nyumbani namatokeo yake wanajikuta wameingia kwenye vishawishi kwahiyo,’’

Hata hivyo amesema uelewa mdogo kwa jamii pamoja na umasikini bado ni tatizo kubwa ambalo lichangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini na kusababisha kuongezeka kwa ufukala katika jamii.

Mkutano huo utadumu ndani ya siku mbili wenye Lengo la kushirikishana hali halisi ya wanawake na watoto wa kike kutokana na thamani ya kimuktadha na tafiti mbalimbali zenye mlengo wa kijinsia, kuthamini kwa pamoja mikakati ya ushawishi na utetezi kwa maboresho ya kisera juu ya masuala ya wanawake na watoto wa kike kiuchumi na kijamii.

Aidha lengo nyingine ni kuunganisha nguvu ya pamoja (tapo) katika harakati za kumkomboa mwanamke na motto wa kike nchni.

Kwa mujibu wa takwimu za taarifa ya utafiti wa hali ya afya Tanzania mwaka 2015 zianonesha asilimia 27 ndoa za utoni,asilimia 33 ukatili wa wasichana, asilimia 10 ukeketajina asilimia 6.3 zinaonesha wanawake wenye HIV/ AIDS.