- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MGOMBEA URAIS NCHINI BRAZIL ACHOMWA KISU HADHARANI (+PICHA 4)
BRAZIL: Mgombea mkuu kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi nchini Brazili Bw.Jair Bolsonaro, amechomwa kisu wakati wa kampeni zake jana Alhamisi sept. 6, mgombea huyo wa mrengo wa kulia alichomwa kisu katika mkutano mkubwa wenye mkusanyiko wa watu wengi katika eneo la kusini mashariki mwa Brazili.
Mwanasiasa huyo ambaye amekua gumzo kwa maoni yake juu ya ubaguzi wa rangi , amepata kura nyingi katika kura za maoni za hivi karibuni.
Kura maoni zinaonesha kuwa atafanya vizuri katika uchaguzi wa urais mwezi ujao na kumpita Mgombea na Rais wa zamani Lula da Silva.
Alichomwa kisu wakati wa mkutano wake wa kampeni wa uchaguzi katika mji wa Juiz de Fora, katika Jimbo la Minas Gerais. na alifanyiwa upasuaji na anaweza kuhamishiwa katika hospitali ya Sao Paulo leo Ijumaa. Hali yake ya afya inaendelea vizuri.
Wapinzani wengi wa Jair Bolsonaro, kutoka mrengo wa kulia na ule wa kushoto, wamelaani shambulio hilo la siku ya Alhamisi usiku, na wameonyesha mshikamano wao dhidi ya kile walisema kitendo cha ujinga na kisiokubalika.
Mgombea huyo wa mrengo wa kulia alichomwa kisu katika mkutano mkubwa wenye mkusanyiko wa watu wengi katika eneo la kusini mashariki.
Mwanasiasa huyo ambaye amekua gumzo kwa maoni yake kuhusu ubaguzi wa rangi, amepata kura nyingi katika kura za maoni za hivi karibuni.
Wauguzi wa hospitali walisema kuwa Bw Bolsonaro amepata jeraha kubwa na limechimba sana kwenye utumbo lakini sasa anaendelea vizuri.
Alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa muda wa masaa baada ya upasuaji, lakini atasalia hospitali hadi siku kumi.
Mshukiwa wa kitendo hicho, Adelio Obispo de Oliveira, anashikiliwa na polisi, kwa mujibu wa chanzo cha polisi.
''kwa bahati mbaya amekua na hali mbaya kuliko tulivyodhani, amepoteza damu nyingi amefika hospitali na damu 10/3 karibu afariki, lakini sasa anaendelea vizuri tafadhali tumuombee'' aliandika katika mtandao wa Twitter.
Wauguzi wa hospitali baadae walisema kuwa bwana Bolsonaro amepata jeraha kubwa na limechimba sana kwenye utumbo lakini sasa anaendelea vizuri.
Alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa muda wa masaa baada ya upasuaji, lakini atasalia hospitali hadi siku kumi.