Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:34 am

NEWS: MGOMBEA URAIS KUTOKA CHAMA CHA KABILA KUTANGAZWA LEO

Muungano wa vyama vinavyounda dola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unatarajiwa kumtangaza mgombea wake wa urais hivi leo Jumatano asubuhi.

Raia wengi wa nchi hiyo wanasuburi kuona ni nani atayepeperusha bendera ya muungano huo wakati huu rais Joseph Kabila ambaye kikatiba hastahili kuwania tena akiendelea kusalia kimya.

Ripoti kutoka jijini Kinshasa, zinasema kuwa viongozi wa muungano huo walikutana jana na kuamua kumweka wazi hivi leo mgombea wake, siku ambayo ndio ya mwisho kwa wanasiasa kurudisha fomu za kuwania urais kwa Tume ya Uchaguzi CENI.

"Washirika wote waliotia saini mkataba wa kuundwa kwa muungano wa vyama vinavyounga mkono serikali (FCC) walikutana Siku ya Alhamisi jioni katika mkutano muhimu huko Kingakati, " waziri ambaye hakutaja jina lake ameliambia shirika la habari la AFP.

“Sio siri tena, itakuwa suala la uteuzi wa mgombea ambaye atapeperusha bendera ya muungano wetu katika uchaguzi wa urais," ameongeza shirika mwingine wa karibu na rais Kabila ambaye pia hakutaja jina lake.

DRC ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi Afrika licha ya rasilimali zake,haijawahi kushuhudia mchakato wa kupeana madaraka kwa amani tangu kupata uhuru kutoka mikononi mwa Ubelgiji Juni 30, 1960.

Tryphon Kin-Kiey Mulumba ambaye ni mshirika wa karibu wa rais Kabila aliwashangaza wengi baada ya kuomba nafasi ya kuwania urais.