- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWAKA ULIOISHI MWENZI SEPTEMBA 2018 UMEONGEZEKA HADI 3.4 %.
DODOMA: Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2018 umeongezeka hadi asilimi 3.4 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Mkurugenzi wa Sensa ya watu na takwimu za jamii kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo,.amesema kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2018 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2018.
Akiendelea kufafanua amesema kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2018 kuechangia na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakulakwa kipindi kinacho ishia mweze Septemba 2018 zikilinganishwa na mwezi septemba 2017.
Licha ya hayo amesema mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Septemba 2018 umeendelea kupungua hadi asilimia 2.0 kutoka asilimia 2.2 ilivyokuwa mwezi Agosti 2018.
Amesema kuwa baadhi ya bidhaa zisizo za chakula ambazo zilizochangia kuongezeaka kwa mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2018 ni pamoja na vileo na bidhaa za tumbaku kwa asilimia 1.9, nguo na viatu kwa asilimia 3.2, vifaa vya matengenezo na ukarabati wa nyumba kwa asilimia 5.2.
‘’Mafuta ya taa kwa asilimia 18.7 mkaa kwa asilimia 11.2 gharama za kumuona daktari hospitali za binafsi kwa asilimia 5.5, dizeli kwa asilimia 19.9 na petrol kwa asilimia 15.8’’ amesema mkurungezi huyo.
Pia amesema hali ya mfumuko wa bei kwa Nchi za Afrika Mashariki kama Nchini Kenya Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwenzi Septemba , 2018 umeongezeka hadi asilimia 5.70 kutoka asimilia 4.04 kwa mwaka ulioishia mwezi agosti 2018.
‘’Kwa upande wa Uganda Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi septemba, 2018 umepungua hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.8 kwa mwaka ulioishia mwezi agosti, 2018’’.