- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MFUMUKO WA BEI NCHINI WASHUKA HADI KUFIKIA ASILIMIA 3.3.
DODOMA: Mfumuko wa bei nchini umeshuka hadi kufikia asilimia 3.3 kwa mwezi Julai 2018 kutoka asilimia 3.4 ya mwezi Juni 2018 ambapo kiwango hiki hakijafikiwa kwa zaidi ya miaka 15.
Taarifa hiyo imetolewa Jijini Dodoma Na kaimu Mkurugenzi ofisi ya taifa ya Takwimu Ephreim Kwesigabo ambapo amesema kuwa hali hiyo inaonyesha kuwa bei za bidhaa hasa zinazotumika kila siku majumbani hazijapanda sana.
Amesema Takwimu hizo zimefanywa kupitia bidaa 278 huku bidhaa zilizochangia kushuka kwa mfumuko wa bei zikiwani unga wa mahindi kupungua kwa 9.5 %,Mtama 17.8%, maharage 5.8% na matunda 22.2%
Pia Kwesigabo amesema hali ya mfumuko wa bei Tanzania inaendana na nchi za Kenya na Uganda ambazo zote zimekuwa katika tarakimu moja.
‘’Nchini Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka julai 2018 umeongezeka hadi asilimia 3.1 kutoka asilimia 2.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Julai 2018’’amesema .
‘’Kwa upande wa Kenya Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai 2018 umeongezeka hadi asilimia 4.35 kutoka 4.28 kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2018’’ameongeza kwa kusema Kwesigabo.