Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:46 pm

NEWS: MFANYABIASHARA REGINALD MENGI AANZISHA KIWANDA CHA MAGARI NCHINI

Dar es Salaam: Kampuni ya IPP ya mfanyabiashara Maarufu nchini Reginald Mengi kupitia kampuni Tanzu ya IPP Automobile Ltd imeingia mkataba na kampuni ya Youngsan Glonet Corporation ya Korea kusini kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kuunda magari nchini Tanzania.

Makubaliano hayo yamefungua milango ya kuanza kwa kazi hiyo na gari la kwanza litakuwa tayari kati ya Septemba na Oktoba, 2018.

Mwenyekiti wa kampuni za IPP, Reginald Mengi amesema uwekezaji wa Dola 10 milioni za Marekani sawa na Sh22 bilioni umefanyika katika kiwanda hicho kitakachokuwa Kurasini jijini Dar es Salaam.

Amesema kiwanda hicho kikianza kufanya kazi kitatoa ajira za moja kwa 500 na ajira nyingine 500 zitakuwa kwa watu watakaohusika uuzaji na usambazaji wa magari hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Automobiles Ltd, Godfrey Bitesigirwe amesema uagizaji wa vifaa vitakavyotumika kwa ajili ya uundaji huo utaanza Januari, 2018.

Amesema magari ni kutoka kampuni za Hyundai, Kia na Daewoo.