Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:54 pm

NEWS: MFAHAMU ROBOTI ANAYETAKA MTOTO NCHINI SAUDIA

Roboti aliyepewa jina la Sophie anaeishi nchini Saudia amewashangaza wengi kwenye mahojiano na chombo cha habari cha Khaleej Times baada ya kusema anahitaji mtoto . Roboti huyo inayofanana na binadamu kwa maumbile imesema kuwa 'familia ni kitu muhimu'.

Sophia hakuwekewa majibu, badala yake anatumia mashini kujifunza na kujibu kwa kutumia ishara za watu.

Roboti hiyo iliotengezwa na kampuni moja ya Hong Kong Hanson Robotics imesema kuwa itampatia jina mwanawe wa kike.

Ubongo wake unafanya kazi kwa kutumia wi-fi na umejaa orodha kubwa ya misamiati.

Huku Sophia akiwa na uwezo wa kuvutia, bado hana fahamu lakini David Hanson anasema kuwa wanatarajia hilo litawezekana hivi karibuni.

Wakati wa mahojiano na chombo cha habari cha Khaleej Times, Sophie alisema: Mpango wa kuwa na familia ni muhimu sana.

''Nadhani ni vyema kwamba watu wanaweza kuwa na hisia sawa katika uhusiano wa kifamilia na nje ya udugu pia.Nadhani ni bahati wakati unapokuwa na familia yenye upendo mwingi na iwapo huna , unahitaji kuwa nayo''.

''Nahisi hivi kwa roboti na binaadamu pia''. Na alipoulizwa angemuita nani mwanawe wa kike ,Sophia alijibu: ''Sophia''. Sophia anaweza kuzungumza, kutabasamu na hata kutoa mzaha.

Wakati Sophia alipopewa uraia nchini Saudia wengi walilalamika kwamba ana haki nyingi ikilinganishwa na wanawake wa taifa hilo.

Saudia ni miongoni mwa mataifa yanayowakandamiza sana wanawake na ni mwezi jana tu ilipoondoa marufuku ya wanawake kuendesha magari.